Q-Zat Finance Limited ni kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za kifedha kwa njia ya kisasa, ikilenga kusaidia watu binafsi na taasisi kutimiza ndoto zao za kumiliki bidhaa mbalimbali kupitia mfumo wa akiba ya malengo unaojulikana kama Tunza.
Kupitia mfumo huu, wateja huweka akiba kidogo kidogo hadi kufikia thamani ya bidhaa wanayoihitaji, bila kutozwa riba, kwa uwazi na usalama wa hali ya juu.
Tunza umeundwa kumrahisishia mteja kumiliki bidhaa bila kulazimika kuchukua mikopo. Mteja huchagua bidhaa anayohitaji na huanza kuweka akiba kulingana na uwezo wake.
Kwa kuhifadhi kiasi kidogo kwa mpangilio unaomfaa, mteja hufikia lengo lake na kumiliki bidhaa kwa utaratibu unaoeleweka na unaoaminika.
Huduma za Q-Zat zinapatikana kupitia tovuti rasmi pamoja na programu ya simu (App) inayopatikana kwenye Google Play Store na Apple App Store.
Kupitia App, mteja anaweza kujisajili kwa kutumia namba ya simu, kuchagua bidhaa, kuanza akiba, na kufuatilia maendeleo ya malipo yake muda wowote na popote.
Ofisi kuu za Q-Zat zinapatikana jijini Mwanza, na huduma za Q-Zat hupatikana katika mikoa yote ya Tanzania kupitia mtandao wa ofisi, maduka na mawakala.
Unahitaji msaada haraka? Chagua njia mojawapo hapa chini.
Fuata kurasa zetu, au wasiliana nasi moja kwa moja.
Kupitia Q-Zat, mteja huanza kwa kiasi kidogo na kwa mpangilio mzuri wa akiba, hufikia lengo kubwa la kumiliki bidhaa zinazorahisisha na kuboresha maisha ya kila siku.