Hati hii inaeleza utaratibu, kanuni na masharti ya matumizi ya huduma ya Tunza inayotolewa na Q-Zat Finance Limited.
Lengo lake ni kumsaidia mteja kuelewa kwa uwazi jinsi huduma inavyofanya kazi, haki zake na wajibu wake.
1. Maelezo ya Huduma
- Tunza ni huduma ya akiba ya malengo kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa.
- Huduma humwezesha mteja kuweka akiba kidogo kidogo hadi kufikia thamani ya bidhaa anayohitaji.
2. Usajili na Ada
- Mteja anajisajili kwa kutoa taarifa sahihi na zinazotambulika.
- Ada ya usajili ni TZS 1,800.
- Hakuna makato ya ziada kwenye akiba ya mteja, isipokuwa pale ambapo kutatolewa taarifa rasmi endapo kutahitajika mabadiliko ya kiutendaji au kisheria.
3. Matumizi ya Akaunti ya Tunza
- Akaunti ya Tunza hutumika kwa manunuzi ya bidhaa pekee.
- Hakuna utoaji wa pesa taslimu (withdraw) unaoruhusiwa kutoka kwenye akaunti ya Tunza.
- Fedha zote zilizowekwa hutumika kukamilisha lengo la bidhaa lililochaguliwa.
4. Uchaguzi wa Lengo (Bidhaa)
- Mteja huchagua bidhaa na kuanza kuweka akiba kulingana na uwezo wake.
- Upatikanaji wa bidhaa utategemea hali ya soko na wasambazaji waliopo.
- Endapo bidhaa haitapatikana, Q-Zat inaweza kupendekeza bidhaa mbadala yenye thamani inayolingana.
5. Kubadilisha Lengo
- Mteja anaweza kuomba kubadilisha lengo (bidhaa).
- Hairuhusiwi kubadilisha lengo kwenda kwenye bidhaa yenye thamani ndogo kuliko lengo la awali.
- Lengo jipya linapaswa kuwa na thamani sawa au kubwa kuliko lengo la sasa.
6. Mteja Kushindwa Kuendelea
- Mteja anatuma ombi rasmi la kusitisha mpango.
- Hakutakuwa na marejesho ya pesa taslimu.
- Mteja atapewa bidhaa inayolingana na salio lililopo kwenye akaunti yake.
- Ombi la kusitisha litafanyiwa kazi ndani ya siku 7 tangu kupokelewa.
7. Sera ya Kuchukua Bidhaa kwa 75%
- Utaratibu wa kawaida: bidhaa hukabidhiwa baada ya kukamilisha malipo ya 100%.
- Kufikisha 75% ya malipo hakuleti uhakika wa moja kwa moja wa kuchukua bidhaa.
- Maombi ya 75% yataangaliwa kwa tathmini ya Q-Zat (historia ya ulipaji, nidhamu ya malipo, historia ya mikopo taasisi nyingine, na uaminifu wa taarifa).
- Mpango wa 75% unatumika kwa bidhaa zenye thamani ya TZS 500,000 au zaidi pekee.
- Bidhaa za ofa (OFAs) au bidhaa zilizo chini ya mpango maalum wa ofa hazihusishwi na utaratibu wa 75%.
- Q-Zat hufanya uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya 75%.
- Mteja atakayekabidhiwa bidhaa kwa 75% ataendelea kukamilisha salio lililobaki kwa mpangilio uliopo.
8. Rekodi na Uthibitisho wa Malipo
- Rekodi za Q-Zat ndizo hutumika kuthibitisha salio na historia ya mteja.
- Mteja anashauriwa kuhifadhi kumbukumbu zake za miamala.
9. Mawasiliano
- Q-Zat inaweza kuwasiliana na mteja kupitia simu, SMS, WhatsApp, barua pepe au App.
- Mawasiliano hutumika kutoa taarifa muhimu kuhusu akaunti na huduma.
10. Faragha na Usalama wa Taarifa
- Taarifa za mteja huhifadhiwa kwa usalama na kutumika kwa madhumuni ya utoaji wa huduma.
- Taarifa zinaweza kutumika kwa uthibitisho wa miamala na uendeshaji wa huduma ya Tunza.
11. Haki na Majukumu ya Q-Zat
- Q-Zat inaweza kusimamisha akaunti endapo kutabainika matumizi yasiyo sahihi au taarifa zisizo sahihi.
- Q-Zat inaweza kuomba uthibitisho wa ziada inapohitajika kwa usalama wa mteja na mfumo.
12. Mabadiliko ya Masharti
- Masharti haya yanaweza kufanyiwa maboresho ili kuboresha huduma.
- Mabadiliko yatatolewa taarifa kwa mteja kupitia njia rasmi.
13. Sheria Inayotumika
- Huduma ya Tunza inaendeshwa kwa kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
14. Utatuzi wa Migogoro
- Changamoto au mgogoro utaanza kutatuliwa kwa mazungumzo na maelewano.
- Ikiwa haitapatiwa suluhisho, hatua za usuluhishi zitazingatiwa.
- Endapo bado haitatatuliwa, suala litapelekwa kwenye mahakama zenye mamlaka nchini Tanzania.
Sehemu ya Sahihi iko upande wa kulia. Jaza jina, account number, kisha usaini ili kupakua PDF.