logo Tumekupata


DHAMIRA YETU
Ni kuwasaidia wateja wetu kupata bidhaa za ndoto zao kwa gharama nafuu, kuokoa pesa na muda wao.

TUNACHOTATUA:
Tunarahisisha njia ya watu kupata bidhaa za kielektroniki wanazotamani kwa gharama ya chini na kuwafikishia bila malipo. Tunauza bidhaa zetu mtandaoni kupitia tovuti yetu, na programu yetu ya android (android App). Tuna wawakilishi wa mauzo waliotawanyika katika mikoa na miji tofauti ambao watafikisha bidhaa mlangoni kwako. Tuna njia tatu ambazo unaweza kutumia kupata bidhaa unayotaka;

~i. Lipa kianzio 50% (nusu bei) ya bei ya bidhaa na upate bidhaa, pesa inayobakia lipa kidogokidogo kwa utaratibu ndani ya miezi mitatu.
~ii. Lipa gharama yote ya bidhaa na upate bidhaa kwa kufikishiwa mlangoni kwako, na
~iii. Kwa kuwekeza pesa kidogokidogo ndani ya muda maalum, na baada ya kukamilisha gharama ya kifaa unapata bidhaa yako.

Ni bei nafuu kununua bidhaa kutoka kwetu kuliko kununua aina hiyohiyo ya bidhaa kwenye duka la kawaida. Tuna programu ya android ambayo inarahisisha michakato yote; pakua Play Store au App Store

BIDHAA ZETU:
Duka letu la mtandaoni linashughulika na bidhaa za kielektroniki pekee kwa sasa. Lakini kumbuka kwamba kampuni yetu inapanua wigo wake kila siku. Tunalenga kuleta suluhisho la utoaji wa huduma ya kufikishiwa kwa haraka zaidi na kwa usalama kwa bidhaa mbalimbali huku tukizingatia ubora wa juu. Tembelea ukurasa wetu wa bidhaa ili kuperuzi bidhaa zinazopatikana au kwa kupakua programu yetu, ambapo pia utapata taarifa ikiwa kuna bidhaa mpya zimeongezwa na ikiwa kuna punguzo na ofa mbalimbali.

KWANINI UNUNUE KUTOKA KWETU?
(FAIDA).

i. Unaokoa muda wako
Huna haja ya kwenda kwenye maeneo ya maduka kutoka duka moja hadi lingine kutafuta bidhaa unayotaka; unaweza kutembelea duka letu kwa njia ya mtandao hata ukiwa safarini. Peruzi bidhaa ukiwa kwenye sofa, ofisini, au njiani kuelekea kazini kwako au wakati ukirudi nyumbani; vyovyote vile.
ii. Unaokoa pesa zako.
Usiwaze kuhusu gharama za usafiri kwa bidhaa unayotaka kununua, pamoja na kwamba unanunua bidhaa zetu kwa punguzo pia hugharamii chochote kuhusu usafiri, usafiri ni juu yetu.
iii. Unapata ubora unaotaka
Tunazingatia kukupa bidhaa bora, bidhaa ambayo hutajuta kumiliki.
iv.Usalama kwa pesa zako.
Pesa yako uliyoipata kwa ugumu haiwezi kupotea kwa kukupa ubora duni, tunaheshimu pesa yako; bidhaa zetu zina waranti. Unaweza kurejesha ubadilishiwe au kurejeshewa pesa, kulingana na masharti ya udhamini wa bidhaa. Unalipa kidogo lakini unapata zaidi (thamani). Unapata bidhaa kwa gharama ya punguzo lakini ubora haupunguzwi kamwe.
v. Unapata bidhaa mapema zaidi
Badala ya kusubiri kupata kiasi chote cha pesa kwaajili ya bidhaa, unaweza kulipa utangulizi 50% (nusu bei) na kupata bidhaa. Kiasi kinachobaki kulipwa kupitia mpango rahisi tunaokupa. Kuhusu ufikishiwaji unapata bidhaa ndani ya masaa 24 kwa walio ndani ya Mwanza na hadi masaa 48 ukiwa mikoa mingine Je, ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu huduma zetu au una swali? Wasiliana na huduma kwa wateja kupitia simu namba +255759903777 au kwa whatsapp